Mkataba wa Kupangisha Nyumba — Kiolezo cha Bure (PDF na Word)
Kiolezo kamili cha Kiswahili kwa nyumba, chumba au fremu ya biashara: kodi, amana, muda, huduma, masharti, sahihi na mashahidi. Pakua, jaza, chapisha.
Wengine huuita mkataba wa pango, mkataba wa upangaji, mkataba wa kupanga nyumba au kwa kifupi mkataba wa nyumba. Ni hati ileile: makubaliano ya maandishi kati ya mwenye nyumba (mpangishaji) na mpangaji. Mfano huu unaweza kuutumia kama ulivyo au kuubadilisha kwenye Word.
Nyumba Zangu inatengeneza mkataba, mpangaji anausaini kwenye simu yake, na unapata PDF. Bure.
Kiolezo chenyewe
Jaza sehemu zenye nukta. Kila upande (mwenye nyumba na mpangaji) ubaki na nakala iliyosainiwa.
MKATABA WA KUPANGISHA NYUMBA
(Nyumba / Chumba / Fremu ya biashara)
Mkataba huu umefanywa leo tarehe mwezi mwaka , kati ya:
Mwenye nyumba
Jina kamili:
Namba ya NIDA: Simu:
Anwani:
Mpangaji
Jina kamili:
Namba ya NIDA: Simu:
Kazi / Biashara:
1. Kinachopangishwa
Mwenye nyumba anampangisha mpangaji nyumba / chumba / fremu ya biashara (futa kisichohusika) namba kilichopo Mtaa , Kata , Wilaya , Mkoa .
2. Muda wa mkataba
Mkataba huu utaanza tarehe na kuisha tarehe (miezi ). Unaweza kuongezwa kwa makubaliano ya maandishi ya pande zote mbili.
3. Kodi
Kodi ni TZS kwa mwezi (kwa maneno: ). Italipwa kila miezi , kabla ya au tarehe ya mwezi, kwa njia ya taslimu / M-Pesa / Mixx by Yas / Airtel Money / HaloPesa / benki (futa isiyohusika). Malipo ya awali: miezi , jumla TZS . Kila malipo yatatolewa risiti.
4. Amana (dhamana)
Mpangaji amelipa amana ya TZS . Itarudishwa ndani ya siku baada ya mkataba kuisha na nyumba kukabidhiwa, baada ya kutoa gharama za uharibifu (kama upo) na madeni yaliyobaki.
5. Huduma
Umeme (LUKU): Maji:
Taka: Ulinzi:
(Andika nani analipa: mwenye nyumba au mpangaji.)
6. Masharti
- Kuchelewa kulipa kodi kwa zaidi ya siku kutasababisha adhabu ya asilimia ya kodi ya mwezi huo.
- Mpangaji hataruhusiwa kupangisha tena (sub-let) wala kukaribisha wakazi wengine wa kudumu bila idhini ya maandishi ya mwenye nyumba.
- Uharibifu wowote wa makusudi au wa uzembe utakaosababishwa na mpangaji au wageni wake utagharamiwa na mpangaji.
- Mpangaji hatafanya mabadiliko ya kimuundo (kuta, milango, umeme, mabomba) bila idhini ya maandishi.
- Mwenye nyumba ana haki ya kukagua baada ya kutoa notisi ya saa 24, isipokuwa dharura.
- Matengenezo makubwa (paa, kuta, mabomba makuu) ni jukumu la mwenye nyumba; madogo ya kila siku ni ya mpangaji.
- Mpangaji atatunza usafi wa nyumba na maeneo ya pamoja, na atafuata sheria za mtaa na za nchi.
- Kwa fremu ya biashara: biashara inayoruhusiwa ni ; mpangaji atakuwa na leseni na vibali vyote vinavyohitajika.
7. Kuvunja mkataba
Upande wowote unaweza kuvunja mkataba kwa kutoa notisi ya maandishi ya siku . Kodi iliyolipwa kabla kwa kipindi ambacho mpangaji hatakaa itarudishwa / haitarudishwa (futa isiyohusika).
8. Migogoro
Mgogoro wowote utasuluhishwa kwanza kwa mazungumzo. Ikishindikana, utapelekwa kwenye vyombo vinavyohusika, ikiwa ni pamoja na Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya.
9. Masharti ya ziada
Mambo ya kuzingatia kabla ya kusaini
- Kila upande uonyeshe kitambulisho (NIDA) na mbaki na nakala zake.
- Pigeni picha za hali ya nyumba siku ya kuingia — kuta, sakafu, milango, vyoo. Zinasaidia wakati wa kurudisha amana.
- Andikeni namba ya mita ya LUKU na ya maji, na salio lake siku ya kuingia.
- Kiasi cha kodi kiandikwe kwa namba na kwa maneno.
- Kila malipo yapewe risiti — tumia kiolezo chetu cha risiti au app.
- Kila upande ubaki na nakala iliyosainiwa.
Maswali yanayoulizwa mara nyingi
Je, mkataba wa kupangisha nyumba lazima uandikwe?
Makubaliano ya mdomo hutumika sana, lakini mkataba wa maandishi ndio ushahidi bora pale mgogoro unapotokea: unaonyesha kodi, muda, amana na masharti mliyokubaliana. Ni vizuri kila upande ubaki na nakala yake.
Amana (dhamana) ya nyumba ni kiasi gani?
Hakuna kiwango kimoja; ni makubaliano kati ya mwenye nyumba na mpangaji. Andika kiasi, na jinsi kitakavyorudishwa mkataba ukiisha, kwenye mkataba wenyewe.
Naweza kutumia kiolezo hiki kwa fremu au chumba cha biashara?
Ndiyo. Chagua "fremu ya biashara" kwenye kipengele cha 1 na jaza sharti la 8 (aina ya biashara na leseni).
Mkataba wa pango na mkataba wa kupangisha nyumba ni kitu kimoja?
Ndiyo. Mkataba wa pango, mkataba wa upangaji, mkataba wa kupanga nyumba na mkataba wa kupangisha nyumba ni majina tofauti ya hati ileile: makubaliano ya maandishi kati ya mwenye nyumba na mpangaji kuhusu kodi, muda na masharti.
Naweza kupata mfano (sample) wa mkataba wa nyumba wa kujaza?
Ndiyo. Ukurasa huu una mfano kamili wa Kiswahili. Pakua PDF uuchapishe na kuujaza kwa mkono, au pakua Word (.docx) ubadilishe maneno kabla ya kuchapisha.
Je, sahihi ya kidijitali inakubalika?
Tanzania, Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya 2015 inatambua sahihi za kielektroniki. Kwa mikataba muhimu, wasiliana na mwanasheria kuhusu hali yako.
Kiolezo hiki ni cha jumla na si ushauri wa kisheria. Kwa mikataba mikubwa au yenye masharti maalum, wasiliana na mwanasheria.