Nyumba Zangu
Wapangaji, mikataba na kodi mahali pamoja. Jua nani amelipa, nani anadaiwa, na unadai kiasi gani — kwa mguso mmoja.
Imetengenezwa kwa ajili ya wamiliki wa nyumba Tanzania — kwa Kiswahili, na kwa jinsi biashara inavyofanyika hapa.
Nyumba za kawaida, apartment, maduka, ofisi na compound. Kila chumba na kodi yake.
Wamepangwa kwa nyumba. Piga simu au tuma WhatsApp moja kwa moja kutoka kwenye app.
Tengeneza, saini na hifadhi mkataba ndani ya app. Hakuna karatasi wala kupoteza nakala.
Rekodi malipo, toa risiti yenye namba, na fuatilia madeni kwa kila mpangaji.
Mpangaji anatuma ombi, wewe unaona na kubadilisha hali hadi limekamilika.
App inakukumbusha kabla mkataba haujaisha — siku 30, 15, 7 na 3.
Wewe na mpangaji mnalipana kama mlivyozoea. App inatunza kumbukumbu tu — ndiyo maana ni rahisi na salama.
Si mwenye nyumba pekee. Mpangaji anaingia kwa akaunti yake na kuona mambo yake mwenyewe.
Pakua, ongeza nyumba yako ya kwanza, kisha waalike wapangaji wako.