Nyumba Zangu › Risiti ya malipo ya kodi
Risiti ya Malipo ya Kodi ya Nyumba — Kiolezo cha Bure (PDF)
Risiti rahisi ya Kiswahili kwa kodi ya nyumba, chumba au fremu. Risiti mbili kwa ukurasa mmoja wa A4: moja kwa mpangaji, nakala moja kwako.
Au mtumie risiti kwa WhatsApp, papo hapo
Pakua app
Nyumba Zangu inatoa risiti yenye namba ya kipekee kila unaporekodi malipo, na salio linalobaki. Bure.
Kiolezo chenyewe
RISITI YA MALIPO YA KODI
Namba ya risiti: Tarehe:
Nimepokea kutoka kwa (mpangaji):
Kiasi: TZS (kwa maneno: )
Malipo ya kodi ya mwezi / miezi:
Nyumba / chumba / fremu: Mahali:
Njia ya malipo: Taslimu / M-Pesa / Mixx by Yas / Airtel Money / HaloPesa / Benki Namba ya muamala:
Kodi ya mwezi: TZS Salio linalodaiwa: TZS
Aliyepokea (mwenye nyumba) — jina na sahihi
Aliyelipa (mpangaji) — jina na sahihi
Kwa nini kila malipo yapate risiti?
- Ushahidi kwa pande zote mbili. Mpangaji anathibitisha amelipa; mwenye nyumba anathibitisha amepokea kiasi gani.
- Malipo ya sehemu yanaonekana. Salio linaandikwa, kwa hiyo hakuna ubishi mwisho wa mwezi.
- Amana na kuondoka. Mpangaji akiondoka, risiti zinaonyesha kama kuna deni kabla ya kurudisha amana.
- Hesabu zako za mwaka. Zinakusaidia kujua mapato halisi ya nyumba zako.
Namna ya kujaza
- Kila risiti ipewe namba inayofuata (mfano 001, 002…) ili kusiwe na mbili zinazofanana.
- Andika kiasi kwa namba na kwa maneno.
- Kwa malipo ya simu au benki, andika namba ya muamala.
- Kama amelipa sehemu, andika salio linalodaiwa.
- Mpe mpangaji risiti, na wewe baki na nakala.